Michezo

Yanga yainyuka Al Ahly ya Misri bao 1 – 0

Nadir Haroub Kanavaro Jumamosi hii ameitoa kimasomaso Yanga kwa kuifungia bao moja na la ushindi dhidi ya klabu ya Al Ahly ya Misri kwenye mechi iliyofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Shabiki namba moja wa Yanga akishindwa kuamini kama mchezo umeisha kwa goli 3-3.

Hiyo ilikuwa ni mechi ya kwanza kati ya timu hizo kwenye hatua ya timu 32 ya mabingwa wa Afrika. Nadir alifunga bao hilo katika dakika ya 82, dakika tu 8 kabla ya kumalizika kwa mechi hiyo.

Mechi ya pili kati ya timu hizo itachezwa Jumapili ijayo jijini Cairo, Misri. Hata hivyo mchezo huo uliingia matatani kipindi cha pili baada ya mashabiki kurusha chupa uwanjani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents