Michezo

Yanga yaramba dume

yanga-logo1

Timu ya soka ya Dar –Es-Salaam Young Africans almaarufu kama Yanga leo jioni imeweza kuwapa raha mashabiki wake kwa kuwafunga  goli moja bila wekundu wa Msimbazi  hivyo  kuwanyamazisha kabisa watani wao simba.

 

 

Bao hilo lilipatikana katikati ya kipindi cha pili lililofungwa na mchezaji wa kimataifa kutoka Zambia Davis Mwape lilitosha kabisa kukata ngebe za Watani wao Simba ambao waliujaza uwanja mkuu wa taifa kwa wingi kupita Yangawakiamini watashinda mchezo huo wa ligi kuu ya bara yaani Vodacom Premier League.

yanga_simba_muda
(Mwanadada aliyeonyesha ujuzi wake katika kuuchezea mpira)

 

Mpambano huo ambao ulianza saa kumi na nusu alasiri ulianza kwa taratibu kwa timu zote mbili kusomana lakini walikuwa ni Simba ambao walionekana kukamia zaidi kwa kushambulia zaidi dakika kumi za kwanza na Yanga wakashika kasi kuelekea dakika za Mapumziko.

Hadi mapumziko si simba wala Yanga aliyeona lango la mwenzake.

yanga_simba_umati_wa_saa

Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kumwingiza Haruna Moshi Boban ambaye alileta uhai katika safu ya kiungo ya timu hiyo na kufanya pambano hilo kuwa kali na la kusisimua kwa wachezaji wa pande zote mbili za Simba na Yanga kujitahidi kuonyesha uwezo zaidi.

Hata hivyo alikuwa mchezaji wa Kiunyarwanda Haruna Nzoyimana ambaye alionekana kung’ara zaidi kwa kuichachafya ngome pamoja na kutawala dimba la kati na kufanya wachezaji wa samba kumfanyia rafu za mara kwa mara ili kumdhibiti.

Na katika kuonyesha Nzoyimana alikuwa akiharibu mambo timu ya Simba iliingiza viuongo watatu ambao wote hawakufurukuta kwa mchezaji huyo wa Kinywaranda ambaye alickuwa nyota wa mchezo wa leo baina ya watani hao wa Jadi Simba na Yanga.

yanga_simba_umati

Hata hivyo Simba itabidi ijilaumu yenyewe kwa safu yake ya ushambuliaji kuonekana kuwa butu kwani walikosa nafasi nyingi za wazi, nyingi zikipotezwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia Felix Sunzu.n

Kabla ya kipindi cha pili mashabiki waliofika uwanja mkuu wa taifa walipata burudani ya aina yake pale mwanadada aliyevalia sketi nyeupe na blauzi ya mauamaua akiwa miguu peku alipoingia uwanjani na kuonyesha uwezo  mkubwa wa kucheza na mpira kama wafanyavyo wachezaji wa Ki brazil na kusababisha kushangiliwa na maelfu ya mashabiki wa simba na Yanga ambao walimtunza pesa nyingi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents