Michezo

Yanga yasajili Mbrazili wa pili, Geilson Santos Santana ‘Jaja’

Mshamabuliaji Geilson Santos Santana “Jaja” raia wa Brazil leo amesaini mkataba wa miaka miwili (2014-2016) kuitumikia timu ya Young Africans.

jajacontr
Jaja akipokea nakala ya mkataba wake kutoka kwa Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu

Katibu mkuu wa Young Africans Beno Njovu amesema usajli wa Jaja unakua ni wa pili msimu huu kwa wachezaji wa kimataifa baada ya awali kumsajili kiungo mshambuliaji Andrey Coutinho ambaye pia ni raia wa Brazil.

“Kazi yetu uongozi ni kutekeleza maelekezo ya kocha mkuu pamoja na benchi la ufundi, walitoa mapendekezo ya usajili kabla hawajaanza kazi na mengine baada kuwasili yote tunajitahidi kuyatekeleza ili kila kitu kiende safi” alisema Beno.

Jaja ambaye alizaliwa tarehe 21 Septemba 1985 na kukulia katika mji wa Aracaju nchini Brazili mpaka anasajiliwa na timu ya Young Africans alikuwa akiichezea timu ya Itabaina FC iliyopo nchini Brazil.

Mshambuliaji huyo mwenye mwili uliojaa vizuri tayari alishaanza mazoezi tangu katikati ya wiki iliyopita chini ya Kocha Mkuu Marcio Maximo na msaidizi wake Leonado Neiva ambao wanaendelea kukinoa kikosi cha Young Africans kwa ajili ya michuano mbalimbali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents