Michezo

Yanga yashindwa kufuzu hatua ya 16 bora, yaondolewa kwa matuta na Al Ahly

Timu ya Yanga usiku wa Jumapili imeshindwa kuendeleza ushindi iliyouanza jijini Dar es Salaam, baada ya kuondolewa na Al Ahly kwa matuta. Hadi mpira unaisha, Al Ahly walikuwa wanaongoza kwa bao moja kwa bila lililofungwa na Sayed Moawad kwenye dakika ya 71na hivyo kulazimisha upigwaji wa penati.

alahly4

Ahly imefanikiwa kushinda kwa penati 4 kwa 3. Wachezaji wa Yanga waliofunga penalti ni Didier Kavumbagu, Emmanuel Okwi na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wakati Oscar Joshua, Mbuyu Twite na Said Bahanuzi wakikosa mikwaju hiyo.

Mechi hiyo imechezwa kwenye uwanja wa Max uliopo jijini Alexandria, Misri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents