Yanga Yatuma Majina CAF

Mabingwa watetezi wa soka wa Tanzania Bara, juzi walituma orodha ya wachezaji wake itakaowatumia katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika. kati ya wachezaji 28, wanne ni wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili.

Mabingwa watetezi wa soka wa Tanzania Bara, juzi walituma orodha ya wachezaji wake itakaowatumia katika mashindano ya Klabu Bingwa. Kati ya wachezaji 28, wanne ni wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili.

Wachezaji hao wapya ni pamoja na Michael Baraza aliyesajiliwa kutoka katika klabu ya RSM ya Malaysia, Ally Msigwa, Steven Marashi na Iddi Mbaga ambao walikuwa katika timu yao ya vijana.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela alisema jana kuwa majina ya wachezaji wa Yanga na Prisons itakayoshiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho yalitumwa katika Shirikisho la soka Afrika (CAF) mwishoni mwa wiki ikiwa ni ndani ya muda uliopangwa wa kuwasilisha majina bila ya kupigwa faini.

Mwakalebela aliyataja majina ya wachezaji wengine wa Yanga watakaocheza katika mashindano hayo ya CAF kuwa ni Juma Kaseja, Nurdin Bakari, George Owino, Athumani Iddi `Chuji`, Wisdom Ndlovu, Geofrey Bonny, Castory Mumbala, Jerry Tegete, Gaudence Mwaikimba, Abubakar Ntiro, Fred Mbuna, Benard Mwalala, Shamte Ally na Mrisho Ngassa.

Wachezaji wengine ni Amir Maftah, Obren Curkovic, Shadrack Nsajigwa, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Boniface Ambani, Kigi Makassi, Hamisi Yusuph, Vicent Barnabas na Abdi Kassim’ Babi’.

Mwakalebela aliwataja wachezaji wa Prisons waliosajiliwa kwa ajili ya mashindano ya CAF kuwa ni Nelson Kimathi, Said Mtupah, Ramadhani Katamba, Aloyce Adamu, Laurian Mpalile, Mbega Daffa, Misango Magai, Henry Mwalugala, Oswald Morris, Shabani Mtupah, Lusajo Mwakifamba na Adamu Mtumwa.

Wengine ni Fredy Chudu, Yonah Ndabila, Ismail Suleiman, Lugano Mwangama, Sylvester Kamtande, Xavery Mapunda, John Matei, Ally Yusuph, Thomas Baragula, Roy Shamba, Geofrey Bamba, Sudi Ahadi, Hashim Suleiman, Abdulrahman Matanda, David Mwantika na Patson Chawinga.

Wachezaji wa Yanga, ambao hawako Stars pia wameanza kunolewa na kocha wao mkuu, Dusan Kondic huku pia Prisons nayo ikiwa inajinoa kambini kwake mkoani Mbeya.

Hata hivyo awali, Yanga ilipanga kwenda kuweka kambi Afrika Kusini kujiandaa na mechi hizo za Ligi ya Mabingwa wa Afrika lakini kutokana na wachezaji wake wengi wa kikosi cha kwanza kuwa katika kambi ya Stars lakini programu hiyo ilivurugika.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents