Habari

Yes, Vanessa Mdee ni girlfriend wangu – Jux

Jux na Vanessa Mdee ni mtu na mpenzi wake, imethibitika.

10958676_1630544703840231_923058955_n

Jux amethibitisha uhusiano wake na muimbaji huyo wa ‘Hawajui’ kwenye mahojiano na kituo cha redio cha Kings FM cha mjini Njombe. Kwa kipindi kirefu wawili hao wamekuwa wakikanusha kuwa na uhusiano.

“Nshaconfess siku nyingi tu. Mwanzo nilikuwa nakataa kwasababu ilikuwa bado unajua first time unakutana na mtu na lazima itafika time mtasema now it’s a time naweza nikasema tu tuko hivyo. Mimi sipendi unasema leo hivi halafu kesho yanatokea mambo mengine, lazima uone kwamba sasa naweza nikasema,” alisema Jux.

Katika hatua nyingine muimbaji huyo alizungumzia pia kuhusu nyumba yake.

Muimbaji huyo amekuwa akipost picha ya nyumba yake hiyo yenye ghorofa moja na kuwaacha watu wengi na maswali kibao ni wapi amepata uwezo wa kujenga nyumba hiyo ilhali si msanii aliye busy na show kama wengine na hana biashara kubwa anayoifanya kumwezesha kuwa na utajiri huo. Hata hivyo kupitia mahojiano na mtangazaji wa Kings FM, King Davidy, Jux amesema nyumba ni ndoto aliyokuwa nayo hata kabla hajajulikana kwenye muziki na hadi nyumba hiyo imefika hapo imetokana na desturi aliyokuwa nayo ya kutunza fedha kwa miaka mingi.

11032785_1378816402417374_1118058827_n

“Watu hawawezi kujua mimi nimeanza muda gani hadi kufika pale, unaweza kukuta hata miaka 10 iliyopita. Kwahiyo sio kitu cha jana na ni kitu cha taratibu, unapata laki tano unaweka, unapata milioni mbili.. sababu nyumba haiozi kama chakula, ni kitu ambacho kinaenda taratibu. Sio kama mimi tajiri sana na nina hela, hizo ni dreams tu,” alisema muimbaji huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents