Habari

Young Buck afungwa miaka mitatu jela

Rapper wa zamani wa kundi la G-Unit Young Buck leo (kwa saa za Marekani) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kutokana na kosa la kumiliki silaha.
Young Buck ambaye jina lake halisi ni David Darnell Brown, alikamatwa mwaka 2010 kwa kupatikana na pistol na silaha zingine za hatari.
Kabla ya kukamatwa na silaha hizo rapper huyo mzaliwa wa Nashville alikuwa na kosa jingine la kumchoma mtu kisu.
Hivyo jaji wa mahakama alitoa hukumu hiyo kutumikia kifungo cha miezi 18 jela kutokana na makosa hayo mawili.
Young Buck pia anakabiliwa na kesi nyingine ya kufilisiwa baada ya kuvunjika kwa mkataba na label ya G-Unit Records.
Vidani vya dhahabu na almasi vinavyomilikiwa na rapper huyo vitapigwa mnada na mamlaka ya mapato ya nchini Marekani IRS, July 26.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents