Soka saa 24!

Young Chalz show zao kutoa sadaka kwa yatima

chaz_face
Mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya  na Meneja wa kundi la Young Chalz, Ezza Chali ‘Zachaa’  ameongea na Bongo5 na kusema kundi la Young Chalz ambalo kwa sasa linatamba na wimbo wa Dezodezo, litakuwa likifanya matamasha kwaajili ya kuchagia watoto yatima.

Zachaa amesema kwamba katika kila tamasha watakalofanya, basi watakuwa wakitoa asilimia kumi ya mapato ya siku hiyo, na kutembelea kituo chochote cha watoto yatima na kutoa msaada huo wa kifedha au kuwanunulia vitu.

Zachaa amesema kundi lake linaundwa na wasanii watano, akiwemo Master Du, Dexo Chaa, Tammy, Jembe na My Selfu ambao wamefanya vizuri katika wimbo hiyo.

Amesema wasanii hao hawawezi kufanya kazi sehemu yoyote bila ya makubalino kati yake na huyo anayeomba kushirikisha, aidha amesema pia wanazingatia ubora wa kazi anayotaka kwenda kufanya kama ni nzuri au inazingua.

Pia amesema msanii wa kundi hilo, haruhusiwi kufanya kazi sehemu yoyote nje  ya kundi, kutokana na mkataba huo.

{hwdvideoshare}id=1567|width=400|height=300|tpl=playeronly{/hwdvideoshare}

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW