Burudani

Young Dee ajivunia kupewa jina na Madee

Msanii wa muziki kutoka label ya King Cash, Young Dee aka rapa paka amedai jina ambalo analitumia kwa sasa Young Daresalama alipewa na msanii Madee Ali ambaye pia ni bosi ya Tip Top Connection.

Rapa huyo ambaye yupo mkoani Shinyanga kwaajili ya Tour ya BBM, amedai Madee ni moja kati ya watu wake wa karibu ambao wakati mwingine humshauri mambo mengi kuhusu muzuki wake na maisha kwa ujumla.

“Kitu ambacho watu hawakijuhi jina ambalo nalitumia kwa sasa hivi Young Daresalama alinipa Madee,” Young Dee aliambia Bongo5. “Kuna siku tulikutana na Madee Clouds FM sasa katika maongezi ya hapa na pale akaniambia wewe unatakiwa uitwe Young Daresalama nikamkubalia na kusema kweli ni jina zuri ambalo kwa sasa nalitumia,”

Rapa huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Bongo Bahati Mbaya, amedai yeye ni mmoja kati ya wasanii vijana ambaye ana waheshimu wasanii wakongwe na kujali nafasi ya kila msanii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents