Burudani

Young Dee azidi kujitetea, ni ishu ya kuvaa sketi

Msanii wa muziki Bongo, Young amenyoosha maelezo baada ya kuonekana akiwa amevaa sketi.

Wiki mbili zilizopita ilivuja katika mtandao picha ya utupu ya Amber Lulu akiwa na Young Dee ambaye alionekana akiwa amevalia sketi. Akizungumza na The Playlist ya Times Fm amesema hakua na maana hiyo kama baadhi ya watu walivyoipokea.

“Ile sketi ni idea ambayo ilikuja na zile picha, mimi ni mtu ambaye napenda kujaribu vitu vingi na off course nimepata comment nyingi nzuri especially nje ya Tanzania, kwamba nimetisha,” amesema Young Dee.

“Lakini tatizo linakuja huku kwetu, unapompelekea mtu ambaye hajakizoea hicho kitu muda wote lazima iwe ni changamoto lakini kwangu ile sketi haikuwa na shida kama ile picha nyingine,” ameongeza.

Young Dee kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Kiutani Utani’ baada ya kusumbua na Bongo Bahati Mbaya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents