Burudani

Young Killer ataja sababu ya wimbo wake ‘Sinaga Swagga’ kukosa majibu kutoka kwa wasanii wengine

Rapper Young Killer amefunguka sababu ya wimbo wake ‘Sinaga Swagga’ kujojibiwa na wasanii wengine.

Killer amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One, amesema wapo wanaojibu chini kwa chini kwa sababu wanaogopa yale mashairi yanayosema “atakayenijibu ni demu wangu na mkiniacha mnaniogopa.”

“Siyo kama umekosa majibu by the way majibu yapo lakini watu wanaogopa kuongea public. Majibu yanakuwa chini chini kwa kuwa nimesema atakayenijibu ni demu wangu na mkiniacha mnaniogopa. Kwahiyo inakuwa ni ngumu kwa mtu kusimama mbele ya hadhara na kutoa majibu,” amesema rapper huyo.

Wimbo huo ulimuingiza Young Killer kwenye matatizo na baadhi ya wasanii wakiwemo Weusi ambapo ndani ya wimbo huo ametajwa Joh Makini na G Nako kutoka kundi hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents