Burudani

Young Killer azijutia baadhi ya collabo alizowahi kufanya

Young Killer amesema kuanzia sasa atakuwa makini katika kuchagua collabo za kufanya kwakuwa nyingi ni miyeyusho mitupu.

AmsrG90eRLHyd4cW9m_K_juWbLQGfOus_lElWONzBWkH

Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa ameamua kufanya hivyo ili kujipa muda wa kufanya mambo yake binafsi kwakuwa baadhi ya wasanii wamempotezea muda.

“Kuna wasanii wengi nimefanya nao collabo lakini naona sioni kama wanatia nguvu kwenye hizo kazi,” amesema Young Killer. “Unakuta msanii anakutafuta ili mfanye kazi, mnapanga vizuri kuhusu kutoka kwa ngoma baada ya hapo unaona yupo kimya tena. Sasa unajua tunaharibiana timing kwa sababu mimi mwenyewe unakuta nimekupa nafasi ya kufanya hivyo kuna kazi zangu nimeweka pembeni ili kupisha yako. Siku zinaenda na kazi hazitoki. Mimi binafsi sijapenda na sasa sifanyi collabo hovyo tena nitakuwa makini na collabo ninazofanya kuanzia sasa,” amesisitiza.

Pia Young Killer amesema anahisi sababu zinazofanya wasanii wengi kuacha kutoa collabo ni kutokana na kuogopa kufunikwa na kuona wataaibika.

“Ukiona msanii umefanya naye collabo halafu haijatoka ujue ameogopa kufunikwa. Mimi sioni sababu ya kukaa na ngoma ndani wakati ilikuwa itoke huku ni kuharibiana timing.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents