Burudani

Young Killer: ‘Muziki ni mkombozi kwenye familia yangu’, haya ni mafanikio aliyoyapata hadi sasa

Kwa Young Kiler muziki ni mkombozi mkubwa si tu kwake binafsi, bali pia kwa familia yake nzima.

11925535_395420703990602_1219673548_n

“Muziki ndio umefanya hadi sasa hivi familia yangu inaendelea kusurvive,” Young Killer alikiambia kipindi cha Chill na Sky.

“Muziki ndio unatoa hata mtaji kwa dada zangu na mama yangu sasa hivi namjengea nyumba na ipo katika hatua nzuri. Sijapata mood ya kuweza kuiweka kwenye mitandao ili watu wapate kuiona kwasababu bado haijakamilika lakini kiukweli mpaka sasa hivi tayari nimeshapiga bati, nishatia milango, bado finishing tu ndogo ndogo.”

Pamoja na hivyo Young Killer amesema muziki umemsaidia yeye mwenye kuendesha mambo yake binafsi ambayo kabla ya hapo alikuwa hawezi kumudu.

Kwa upande wa kusoma, rapper huyo amesema alishindwa kuendelea kutokana na ratiba za chuo kuathiriwa na safari zake za mara kwa mara za kwenda kufanya show.

Sikiliza kipindi hicho hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents