Burudani

Young Killer na mpenzi wake wanashare siku moja ya kuzaliwa, wazungumzia ndoa

Rapper Young Killer Msodoki na mpenzi wake Halimaty, jana wamesherehekea siku yao ya kuzaliwa kwa pamoja. Wote walizaliwa April 13.

11084857_478203119010340_1681365515_n

Young Killer ameiambia Bongo5 kuwa hiyo ni furaha katika maisha yake na kwamba mipango ya ndoa ipo mawazoni mwao.

“Jana tumesherehekea siku ya kuzaliwa mimi na mpenzi wangu Halimaty. Lakini kikubwa zaidi ni kusherehekea siku ya kuzaliwa na mtu ambaye unampenda toka moyoni na toka ninaanza muziki mpaka leo nipo naye,” amesema Killer.

“Hili ni jambo la furaha sana. Masuala ya ndoa bado ingawa kila kitu kinawezekana/ Kuna vitu nahitaji kujipanga zaidi ili kukabiliana na ndoa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents