Burudani

Young Thug ajifananisha na Tupac

By  | 

Rapper Young Thug ameamua kuufahamisha ulimwengu kuwa yeye ndio Tupac mpya baada ya Tupac Amaru Shakur mwenyewe aliyefariki miaka 25 iliyopita.

Thug ambaye Ijumaa iliyopita ya Juni 16 ikiwa ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa marehemu Tupac aliachia albamu yake mpya ya Beautiful Thugger Girls, kupitia mtandao wa Twitter amesema ameamua kufanya hivyo kwa sababu yeye ndio Pac mpya.

“I dropped E.B.B.T.G on 2PAC’S bday because I’m the #newPAC I feel like I am the thug he didn’t get to become #SoImGoinFinishWhatHeStarted??,” ameandika kwenye mtandao huo.

Sio Thug pekee ambaye amejifananisha na Tupac, wengine ni rapper Troy Ave ambaye pia ameachia albamu aliyoipa jina la ‘Nupac’ na Boosie Badazz ambaye pia amewahi kusema albamu yake mpya itaitwa ‘BooPac’.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments