Burudani

Z-Anto akiri kujiondoa Tip Top Connection kulimfanya arudi nyuma kimuziki

Muimbaji wa Bongo Flava, Z-Anto amesema kujiondoa Tip Top Connection ni moja ya sababu kubwa iliyomfanya arudi nyuma kimuziki.

ZAnto

Akiongea na kipindi cha Mseto cha Radio Citizen ya Kenya, muimbaji huyo alisema baada ya kujitoa Tip Top ilikuwa ngumu kwake kusimama kwa miguu yake mwenyewe kwakuwwa alikuwa hajui njia zinazotakiwa kupitwa ili msanii aweze kufanikiwa.

“Nililazimika kushuka kwa sababu hiyo. Lakini nilipokuja kuzigundua zile njia nikaweza kupenya na ngoma binafsi nilijisimamia mwenyewe kwa kila kitu ambayo ndio hiyo Kisiwa cha Malavidavi,” alisema. Aliongeza kuwa kwa sasa hana tatizo na Tip To Connection na kwamba Babutale bado anamhitaji.

“Mpaka kesho (Babu Tale) bado ananipenda. Hata ukimuuliza katika wasanii wake anaowapenda atatajwa wawili asishindwe kunitaja mimi.”

Hata hivyo alisema hana mpango wowote wa kurudi tena kwenye kundi hilo. Msikilize zaidi hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents