Burudani

Z Anto ataja sababu za ukimya wake

Msanii wa Bongo Fleva, Z Anto aliyewahi kufanya vizuri na wimbo ‘Binti Kiziwi’ amesema ukimya wake katika game ulitokana na yeye kuwa na biashara zake nyingine.

Muimbaji huyo amebainisha kuwa alikuwa kimya kutokana alikuwa nje ya sanaa ili kufutilia biashara zake lakini muda si mrefu atarejea.

Z Anto ameendelea kwa kusema hapendi kutoa ngoma kila mara kwa sababu anaogopa kufelisha ngoma zake ila siku akitoa ni wazi atarejea katika nafasi zake.

“Bora nikae miaka mitano au sita lakini nikichomoka nisema bwana nimerudi, sijawahi kufeli katika mashambuilizi ambayo nimeyaandaa ya namna hiyo, kwa sababu nakumbuka nilikaa miaka mitatu sijatoa wimbo lakini nilipokuja kutoka na Kisiwa ikasimama vile vile,” ameiambia E-News ya EATV na kuongeza.

“Nafasi yangu ipo pale pale, na jina langu linakuja kusimama zaidi ya vile kulingana na aina ya ngoma ambazo tayari ninazo,” amesistiza Z Anto.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents