Tupo Nawe

Z Anto azua gumzo mtandaoni kwa kauli yake “Wasanii wakali wote wana majina ya wanyama, sijui mimi nitabatizwa jina gani mwaka huu”

Msanii wa muziki @z_antoofficial amezua gumzo mtandaoni baada ya kauli yake ‘wasanii wote wakali wanatumia majina ya wanyama’ kauli ambayo hakuifafanua zaidi.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo MakoStamina hivi karibuni akiwa katika Interviews na Bongo5TV alionyesha sana kumkubali Diamond Platnumz na kudai kwamba ni msanii mwenye mbinu nyingi za kufanya vizuri kimuziki. “Wasanii wengi wanafeli kwa kumuiga Diamond, huyu jamaa ana mbinu nyingi za kufanya muziki wake kubwa mkubwa, sasa jichanganye akupoteze” alisema Z Anto kupitia mahojiano hayo.

Sasa siku ya jana baada ya kuachia ujumbe huu “2020 #newstar Wasanii wakali wote wana majina ya wanyama #Chui #Simba mwaka huu cjui ntabatizwa jina gan.” watu wengi wamekuwa na maoni tofauti.

Maoni ya mashabiki hao.

Mdathiruahmada3:
Sema Nn We Jamaa, Nakuelewaga Sana yan, Nakukubal kinoma noma ujue🤙

Aishwaryofficial:
Kwan na ww ni msanii mkali?

Officialmudybest:
Me ningependekeza uitwe #CHATU mana uyo nyoka nikiumbe hatari sana aswa akiwa mawindoni

Angeltheflorist:
😂😂😂😂😂😂 jamani Binti kiziwi wako yupoooo ???ule wimbo ebu ufanyie remix ni mzuri sana sanaaaaaaa

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW