Burudani

Z Anto kuachia ‘Mpaka Naogopa’ akiwa na siri mzito ya mapenzi

Baada ya ukimya wa muda mrefu wa msanii aliyewahi kufanya vizuri na wimbo kama ‘Mpenzi Jini’ na nyingine nyingi, Z Anto Jumamosi hii anaachia wimbo mpya ‘Mpaka Naogopa’ ambao ndani yake una mambo mazito aliyewahi kupitia kwenye mahusiano.

Muimbaji huyo aliwahi kufunga ndoa na video queen wa wimbo Binti Kiziwi ambaye kwa sasa anatumikia kifungo China baada ya kukutwa na dawa za kulevya nchini humo.

Z ameimbia Bongo5 kwamba baada kuona mpenzi wake huyo haeleweki, aliachana naye na kuamua kufunga ndoa na mwanamke mwingine.

“Kwa sasa nimeona lakini hivi karibuni aliyekuwa mpenzi wangu wa zamani ambaye amefungwa China amekuwa akiniuliza hili suala na kuoneshwa kuulizwa nalo,” alisema Z.

Aliongeza, “So baada ya kuona hiyo hali na yeye anakaribia kutoka nikaona nieleze namna gani napendwa na mke wangu wa sasa, lakini hili linawatokea watu wengi na wanashindwa kueleza ukweli kwamba kwa sasa nina mwanamke mwingine na kujikuta unasababisha matatizo au ukaaribu maisha yako na familia ambayo umeyajenga kwa miaka mingi,”

Alisema ‘Mpaka Naogopa’ ni wimbo wa mapenzi ambao naeleza jinsi gani napendwa kwa sababu tatizo ambalo linatatiza ndoa nyingi ni kusema ukweli.

Z alisema wimbo huo umendaliwa na producer Mazuu huku video ikiwa imendaliwa na Kwetu S

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents