Burudani

Z Anto kuonyesha fremu zake 70 za biashara, zipo katikati ya Dar

Msanii mkongwe wa muziki, Z Anto wiki ijayo atazionyesha fremu zake 70 za biashara ambazo nimpatia jeuri nje ya muziki.

Akiongea na Bongo5 Jumatano hii meneja wa msanii huyo, Namajojo amedai watafanya tukio hilo kuwathibitishia baadhi ya watu ambao wamekuwa wakibisha na kuona kwamba ni kitu ambacho hakiwezekani.

“Kabla ya kuachia kazi mpya wiki ijayo tutaanza kwanza kuonyesha fremu 70 za Z Anto kwa sababu kuna baadhi ya watu wamekuwa wakizungumza sana kwenye mitandao, ndio zipo hapa Dar es salaam. Sisi tutaonyesha ili mjue Z Anto sio msanii tu bali ni mfanyabishara mzuri sana,”

Katika hatua nyingine meneja huyo amewataka mashabiki wa muziki wa mkongwe huyo kukaa mkao wa kula kwaajili kazi mpya ambazo amedai zinakuja kuleta mapinduzi katika tasnia ya muziki.

Muimbaji huyo ambaye aliwahi kutamba na wimbo kama ‘Binti Kiziwi’ alikuwa nje ya muziki kwa muda mrefu kutokana na shughuli za biashara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents