Michezo

Zahera namna anavyomuona Ajib, awashangaa waandishi ‘Ajib anawashinda akili wachezaji wote wa Tanzania’ 

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga raia wa Kongo, Mwinyi Zahera amemwagia sifa nyota wake Ibrahim Ajib Migomba kwa vile anavyomuona yeye kuwa anakipaji cha hali ya juu na mwenyeakili kuliko wachezaji wote wa Tanzania lakini anashangazwa na waandishi wa habari kutotoa habari hiyo pindi anampomzungumzia na badala yake hutoa kipande  cha video ambacho huonekana akimsema vibaya.

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga raia wa Kongo, Mwinyi Zahera

Zahera ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya timu ya Lipuli FC na kupata ushindi wa bao 1 – 0.

”Nyie waandishi huwa naangalia video zenu wakati ninapofanya mkutano wangu, kila mara mnaachia kipande cha video namsema Ajib vibaya wakati nasema Ajib anawashinda wachezaji wote wa Tanzania akili lakini hata siku moja sikuona mnaachia kipande hicho cha video.”

Mwinyi Zahera ameongeza ”Kila mara mnaachia vitu vya hovyo,  ooo Ajib kocha wake anasema anampa nne kwa nane 4/8 mara Tambwe hivi na hivi wakati nawaambia Ajib ni mchezaji mmoja mwenye akili ya mpira kushinda wachezaji wenu wote wa hapa Tanzania.”

”Ila anapungukiwa na baadhi ya vitu vinavyomfanya yeye kushindwa kuwa mchezaji mkubwa sana na mseme tunashindwa kufunga magoli mengi kwa sababu viungo wetu wale watatu wa katikati hawana ubora wa moja kwa moja kama, Ngasa, Kaseke hawana ubora wa moja kwa moja kwakusema wanaweza kuwatoka wachezaji pinzani na kwenda kushambulia hawana ndiyo inatupelekea sisi kupata ushindi huo.”

”Hakuna hata mwandishi mmoja anayeniuliza kocha mshacheza mechi sita bila kufungwa hata mmoja, ni kila siku Ajib, Tambwe.”

Katika mchezo huo dhidi ya Lipuli FC straika huyo wa Yanga hukuwa kwenye mchezo huo baada ya kupata maumivu ya mgongo ambayo bado anaendelea na matibabu chini ya uangaliazi wa Daktari wa timu ili kuweza kupona haraka na kurejea kwenye majukumu yake.

Hata hivyo Yanga walimaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya beki wao Paul Godfrey kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 82 kufuatia kupata kadi ya pili ya njano.

Msimamo wa ligi baada ya mechi tisa za raundi ya 12.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents