Tupo Nawe

Zaidi ya watu 1,000 wakimbia makazi yao na 60 wafariki dunia kutokana na mafuriko nchini Afrika Kusini

Watu wapatao 60 wamefariki dunia na zaidi ya 1,000 wameyakimbia makazi yao baada ya mvua kali kusababisha mafuriko pamoja na maporomoko ya tope katika eneo la pwani ya mashariki mwa Afrika Kusini. Vifo vingi vimeripotiwa katika jimbo la KwaZulu-Natal.

Mafuriko hayo pia yamesababisha vifo vya watu watatu katika jimbo jirani la Cape Mashariki. Mvua hizo zaidi zimenyesha katika mji wa bandari wa Durban.

Tangu jana shughuli za uokozi zimekuwa zikiendelea.Hapo jana rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alizitembelea jamii zilizoathirika na mafuriko hayo katika jimbo la KwaZulu-Natal.

Anatarajiwa kulitembelea jimbo la Cape Mashariki katika siku zijazo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW