Michezo

Zaidi ya Mataifa 220 kuonyesha pambano la Mayweather na McGregor

Hii leo majira ya alfajiri dunia itakuwa kimya kwa muda kupisha pambano kubwa laaina yake baina ya bondia wa Marekani, Floyd Joy Mayweather Jr  dhidi ya McGregor pigano ambalo linatarajiwa kuonyeshwa na runinga zaidi ya mataifa 220 kwa mujibu wa rais wa Showtime Sports,Stephen Espinoza.

Idadi hiyo ya watazamaji kutoke kote duniani inaweza kuipiku rekodi ya watazamaji ya watu milioni 4.6 iliowekwa wakati wa pigano kati ya Mayweather dhidi ya Manny Pacquiao 2015.

Watazamaji wa pigano hilo nchini Uingereza watalipa pauni 20 kila mmoja lakini wale wa Marekani watalipa pauni 75 kila mmoja.

Fedha hizi zikijumlishwa na mauzo ya tiketi ya kutazama pigano hilo ufadhili na biashara inaweza kuleta kiwango kikubwa cha fedha.

Tiketi pia zinauzwa za kutazama pigano hilo katika vilabu katika mji wa Las Vegas, huku zaidi ya kumbi 400 za filamu pia zikilionyesha pigano hilo.

Hiyo inamaanisha kwamba takriban dola milion 600 zinaweza kupatikana, kiwango kinachokaribia kile cha pigano kati ya Mayweather na Pacquiao.

Mayweather anatarajiwa kujipatia dola milioni 300 huku McGregor akiweka kibindoni dola milioni100.

Kumekuwa na ripoti kwamba Mayweather anaonekana kumpuuzilia mbali McGregor.

Wiki hii wachanganuzi wa mambo wamesema kuwa hatua ya Mayweather kumpuuza mpinzani wake kunaweza kuwa hatari kubwa kwake.

Baba mzazi Mayweather Floyd jr, wiki hii alisema kuwa mwanawe amepoteza uwezo wake mkubwa tangu alipostaafu 2015.

Lakini iwapo atashinda pigano lake la hamsini katika maisha yake ataweza kuipita rekodi iliowekwa na Rocky Marciano ya kushinda mara 49 bila kushindwa.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents