Habari

Zaidi ya watu 890 wauawa nchini DR Congo, siasa na ukabila vyatajwa

Zaidi ya watu 890 wameuawa nchini DR Congo kufuatia kwa vita vya kikabila vilivyodumu kwa siku tatu magharibi mwa nchi hiyo, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa (UN).

Image result for DR CONGO 890 PEOPLE

Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia haki za binadamu, inaeleza kuwa mapigano hayo kati ya jamii za Banunu na Batende yalizuka katika vijiji vinne huko Yumbi.

Idadi kubwa ya wakaazi wa eneo hilo inaarifiwa wameachwa bila ya makaazi.

Ripoti hiyo imesema kuwa zaidi ya nyumba 465 zimeharibiwa, zikiwemo shule mbili za msingi, kituo cha afya, soko na ofisi ya tume huru ya uchaguzi katika eneo hilo, Umoja huo umesema.

Raia walioachwa bila ya makaazi ni pamoja na watu 16,000 waliotafuta hifadhi kwa kuvuka mto Congo hadi katika nchi jirani ya Congo-Brazzaville, umeongeza.

SOMA ZAIDI TAARIFA HIYO->https://www.ohchr.org/EN/NewsEvents/Pages/DisplayNews.aspx?NewsID=24075&LangID=E

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents