Promotion

Zain Corporate Golf Kuanza Kesho

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain, imetoa Sh4milioni kudhamini mashaindano ya gofu ya Zain Corporate Challenge yatakayofanyika kesho kwenye viwanja vya klabu ya Lugalo, Dar es Salaam.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain, imetoa Sh4milioni kudhamini mashaindano ya gofu ya Zain Corporate Challenge yatakayofanyika kesho kwenye viwanja vya klabu ya Lugalo, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa fedha wa Zain, Heiko Schlittke aliwaambia waandishi wa haabri jana kuwa mashindano hayo yana lengo la kuuendeleza mchezo huo.
Alisema watu mbalimbali wanaruhusiwa kushiriki na washindi watapata zawadi mbalimbali ikiwemo tuzo maalum.
“Hatuna budi kuwashukuru wote washiriki wote wa mashindano haya na tuna imani udhamini wetu utafanya mashindano haya kuwa ya kimataifa zaidi na kuongeza chachu ya usshindani pamoja na kupromoti gofu katuika Tanzania,” alisema.
Mashindano hayo ya siku moja, yanatarajia kuanza saa 6:00 mchana yatachezwa katika mfumo wa mtu mmoja mmoja na timu kuwakilishwa na wachezaji wawili,” alisema Schlittke.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents