Promotion

Zain yabadilishwa kuwa AIRTEL

Kampuni ya utoaji huduma na bidhaa za simu ya Zain kuanzia jana jioni ilizinduliwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na kutambulika rasmi kwa  jina la AIRTEL nchini Tanzania baada ya Kampuni hiyo kuuzwa kwa wamiliki wapya wa Bharti Airtel ya nchini  India.

 

Hatua hiyo imekuja kama sehemu ya kuiondoa rasmi kampuni ya zain katika soko la Afrika baada ya kampuni hiyo kununuliwa na wamiliki wapya mwezi wa sita mwaka huu.

Kampuni hiyo ya zain ambayo thamani yake ilikadiriwa kuwa pesa za kimarekani bilioni 2 ilifanyiwa mahesabu na kampuni binafsi ya kifedha ya Brand finance 500 mwaka 2009.

Katika mchakato huo wa kubadili muonekano na kuasili jina jipya la kibiashara, nchi 14 barani Afrika zitaanza kutumia jina jipya la Airtel zikijihusisha kikamilifu na wamiliki wapya wa kampuni hiyo ambao makao makuu yake ni bara asia.

Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa Zain ambayo ilianza kwa kutumia jina la MTC nchini Kuwait kupata jina jipya  la kibiashara kutokana na  kupata wamiliki wapya. Kabla ya kuitwa Zain kampuni hiyo ilikuwa ikitumia jina la Celtel kibiashara kabla ya kununuliwa na mfanyabiashara maarufu Mo Ibrahim.

Kubadilika kwa jina hilo la kibiashara kumefuatia kununuliwa kwa kampuni hiyo ya mawasiliano na kampuni hiyo ya India Bharti Airtel kwa gharama ya pesa za kimarekani bilioni 7 kutoka kwa milionea bwana Sunil Bharti Mittal ambaye ni muanzilishi na mwenyekiti wa kampuni hiyo.

Aidha bado haijajulikana ni kiasi gani hasa kitatumika kuibadili sura  na muonekano wa kibiashara wa kampuni hiyo ingawaje kampuni ya Zain ilitumia zaidi ya bilioni 10 katika kujitangaza upya Tanzania.

Kwa kuinunua Zain kampuni ya Airtel imeweza kuingia katika soko la nchi 14 ikijumuisha nchi za Kenya, Uganda, Madagascar,Zambia, Malawi na Nigeria.

Akizungumzia mabadiliko hayo ya sura na muonekano mpya wa kampuni ya Zain katika soko la Afrika mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Moringa Ogilvy Bw. David Case  ambayo pia ni sehemu ya kampuni Ogilvy Africa kampuni yake itasimamia na kuahidi kuleta mapinduzi katika muonekano wa kampuni hiyo nchini Tanzania.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents