Habari

Zama za kuficha habari zimepita – Kaimu Jaji Mkuu

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amewataka baadhi ya watumishi wa Mahakama nchini kutoficha ukweli wa habari kwa vyombo vya habari ili kuepuka kuvumishwa habari kwa Mahakama ambazo zinapotosha ukweli.


Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma

Agizo hilo amelitoa Kaimu Jaji huyo akiwa mkoani Manyara ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu kuteuliwa kwake ambapo amelenga kusikikliza changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi wa Mahakama.

“Kuna sheria ambayo ilitungwa mwaka jana ya kutoa habari, sheria namba 9 ya 2016 ambayo inasema kila Taasisi iliyoundwa kwa mujibu wa sheria au kwa mujibu wa Katiba, inakuwa na jukumu la kutoa habari, kwa hiyo zile zama za kuficha habari zimepita,” alisema Prof. Juma.

Kwa upande mwingine, Kaimu Jaji Ibrahimu amewataka watumishi wa Mahakama kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na mipaka ya kazi yao na kuyaweka mbele zaidi maslahi ya wananchi.

Hata hivyo Kaimu Jaji huyo amemaliza ziara yake Mkoani humo kwa kuongea na Watumishi wa Mahakama wa kanda hiyo.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents