Burudani

Zamaradi: Babu Tale ndiye aliyenitambulisha kwa Ruge kwa mara ya kwanza (Video)

Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba bado anaumwa na tukio linaloendelea kwa sasa ni Watanzani na marafiki wa bosi huyo kumuombea na kumchangia baada ya gharama ya matibabu kufikia tsh milioni 650.

Clouds TV kupitia kipindi cha Clouds 360 wamekuwa waliwaalika wadau mbalimbali ambao wanaguswa na maisha ya Ruge na kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu mwanaharakati huyo wa muziki wa Bongo Fleva.

Alhamisi hii amealikwa, Zamaradi ambaye ni mama watoto wa Ruge ambapo amefunguka mambo mbalimbali pamoja na namna alivyokutana na bosi Ruge.

“Tulikutana na Ruge kwenye mazingira ya kazi, na mimi nimemjua Ruge kupitia Babu Tale. Tale ndio mtu ambaye alinitambulisha kwa Ruge kwa mara ya kwanza, alinipa namba yake akanimbia mtafute huyu bwana lakini usimwambie kama mimi ndiye niliyekupa namba,” alisema Zamaradi.

Mapema wiki hii Mbaki Mutahaba ambaye ni ndugu za Ruge akielezea kiasi cha fedha ambacho kilitumika toka Ndg Ruge Mutahaba aanze kuumwa.

Unaweza kuendelea kutuma ujumbe wako wa faraja au kutuma chochote kupitia number 0752 222 210 na jina ni Kemilembe Mutahaba au kupitia CRDB Bank account number 0111055925300, 
Dr. Gelase Rwabyo Mutahaba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents