Burudani

Zamaradi Kugombea ubunge

Inasemekana kwamba mtangazaji wa Clouds FM anayekuja kwa kasi Zamaradi Nketema, naye ameamua kwa moyo mmoja kuingia kwenye siasa huku kiu yake ikiwa ni kutinga Bungeni baadaye Novemba mwaka huu wa 2010 kupitia Ubunge wa Viti Maalum CCM.

 

Zamaradi pia amethibitisha kuwa ni kweli amechukua fomu “Ni kweli nimechukua fomu leo (Jumanne) na ninatarajia kurudisha kesho. Siwezi kuongea mengi kwasasa, labda hadi nitakaporudisha fomu. Nitafute kuanzia kesho, na kuendelea, ninaweza kuwa na mengi ya kuongea,” alisema Zamaradi.

Zamaradi anakuwa mtangazaji wa pili wa kituo hicho kurusha karata yake kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya marehemu Amina Chifupa kufanikiwa
kuingia bungeni kwa uteuzi kama anaowania. Bongo5 inaendelea kufatilia habari hii kwa ukaribu zaidi hili kujua mengi kutoka kwa zamaradi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents