AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Zamaradi Mketema azungumzia kilichomfanya aandae filamu ya ‘Kigodoro’ yenye mastaa kama Hemedy, Kajala na Muhogo Mchungu

Mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds TV, Zamaradi Mketema hivi karibuni aliingia msituni kuandaa filamu yake iitwayo ‘Kigodoro’ iliyoshirikisha mastaa wakiwemo Hemedy PHD, Kajala na Muhogo Mchungu.

4a2fc18e3afd11e3aa5922000a1ddaa1_7

Akiongea na Bongo5, Zamaradi alisema aliamua kuandaa filamu hiyo baada ya kuona kuwa filamu nyingi za Tanzania zina hadithi zile zile hivyo alitaka kuja na kitu tofauti.

“Tuna mambo mengi sana ambayo yanaendelea Tanzania ambayo yanaweza kukaa kwenye filamu yakachekesha, yakafurahisha, yakaelimisha. So nikafikiria, nikawaza yale maisha ya uswahilini, watu wanasutana, wanagombana, yale maisha ambayo unakuta chai ipo lakini vitafunio mnajitegemea, nimejaribu kuangaza familia ya aina ile,”alisema Zamaradi.

“Nikatoa idea, nikampa mtu aniandikie script, akaandika script vizuri ndo tukaingia mzigoni.”

Zamaradi amesema hadi sasa gharama aliyoitumia kutengeneza filamu hiyo ni zaidi ya shilingi milioni 16.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW