Soka saa 24!

ZAMBIA: Malalamiko ya wanawake yapelekea serikali kuchunguza kinywaji cha Konyagi, Yadaiwa kuongeza nguvu za kiume

Mamlaka ya Dawa nchini Zambia (ZAMRA) imeanza mchakato wa kufanyia utafiti kilevi cha konyagi kutoka Tanzania ili kuthibitisha kama kweli kinaongeza nguvu za kiume kama kinavyolalamikiwa na wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kiongozi wa Mamlaka hiyo Jana Jumatatu, Jerome Kanyika amesema kuwa kumekuwa na malalamiko mengi juu ya kinywaji hicho kutoka kwa wanandoa.

Jerome amesema malalamiko mengi yametoka kwa akina mama ambao wamedai wanaume wao huwa wanawasumbua kwa kuchelewa kufika kileleni pindi wanapolewa pombe hizo.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail Zambia, Limeeleza kuwa kinywaji hicho kwa sasa kinatumiwa hata na watu wasiokuwa wanywaji ni baada ya tetesi hizo kuibuka.

Baadhi ya Wanaume waliohojiwa na gazeti hilo wamekiri kuwa waliwahi kutumia kinywaji hicho kwa lengo la kuongeza nguvu.

Ripoti ya ZAMRA inatarajiwa kutoka mwishoni mwa mwezi huu.

Chanzo: http://www.daily-mail.co.zm/sex-boosting-spirit-reported-to-zamra/

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW