Habari

Zamu yangu kumuunga mkono mke wangu – Dkt Kikwete

Rais Mstaafu wa awamu wa nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amesema ameshuhudia kiapo cha Mke wake, Mama Salma Kikwete baada ya kuteuliwa hivi karibuni kuwa mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais huyo mstaafu alifuatana na baadhi ya familia yake na kushuhudia mkewe akila kiapo hicho katika bunge lililoanza leo mjini Dodoma huku akisema kuwa ni zamu yake sasa kumuunga mkono mkewe.

“Leo asubuhi nimeshuhudia kiapo cha Mke wangu Mhe. Salma Rashid Kikwete kuwa Mbunge wa Kuteuliwa Bungeni Dodoma.Ni zamu yangu kumuunga mkono,” ameandika Dkt Kikwete kupitia akaunti yake ya Twitter.

Dkt Kikwete aliingia ndani ya bunge akishangiliwa na idadi kubwa ya wabunge wa bunge hilo.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents