Zantel watua Barcelona

Zantel watua Barcelona
Mabingwawapya wa Ulaya, klabu ya Barcelona ya Hispania wameingia
mkataba na Kampuni ya simu ya Zantel ambao watakuwa washiriki rasmi wa
mawasiliano wa kimataifa wa klabu hiyo. Zantel wameingia mkataba wa
miaka minne na Barcelona ambao utawawezesha wateja wao kuungana na
wachezaji maarufu wa klabu hiyo na kupata fursa ya kushuhudia timu hiyo
ikicheza moja kwa moja katika Uwanja wa Camp Nou

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Zantel, Dar es Salaam jana
mkataba huo wa ushirikiano na Barcelona na kupitia kampuni mama ya
Zantel, Etisalat na utaiwezesha kampuni hiyo kujiita ‘Mshirika Rasmi wa
Kimataifa wa FC Barcelona’ na kampuni zake tanzu ambazo ziko katika
nchi 17 duniani ikiwamo Zantel ya hapa nchini.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa kutokana na ushirika huo Zantel itapata
fursa ya kushirikiana na Barcelona katika shughuli za kimasoko zikiwamo
kujitangaza na kufanya promosheni za pamoja, haki za kutumia picha na
nyaraka zao kwenye mtandao wa klabu hiyo. “Soka ni mchezo maarufu zaidi
duniani, kutokana na kampuni yetu huduma zake kuwa zimeenea katika
ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ushirika huu na timu maarufu duniani
kama Barcelona ni uamuzi sahihi ambao utasaidia kukuza jina la kampuni
yetu,” alisema Essa Al Haddad, Ofisa Masoko Mkuu wa Kundi la Kampuni za
Etisalat.

Haddad aliongeza kuwa ushirika huo pia utafungua njia nyingi za
kuwezesha kukidhi matakwa na kukonga nyoyo za wateja wao wapatao
milioni 80 duniani hivyo, kama kampuni mama wanafurahi kuona Zantel
ikishiriki kikamilifu kuhakikisha ushirika huo unawanufaisha wateja wa
Zantel Tanzania. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Zantel,
Noel Herrity, alisema kuwa ana hakika kuwa ushirika huo na Barcelona
utaongeza thamani kwenye huduma wanazotoa kwa wateja wao ukizingatia
kuwa soka ndio mchezo unaopendwa zaidi na Watanzania.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents