Michezo

Zanzibar Heroes yafa kiume Kenya, Yatoa somo kwa ‘vibonde’ Kilimanjaro Stars

Timu ya mpira wa miguu ya Zanzibar Heroes imefanikiwa kushika nafasi ya pili ya michuano ya CECAFA baada ya kukubali kichapo cha goli 3-2 kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya kwenda sare ya goli 2-2 kwa kwa dakika 120.

Zanzibar Heroes

Licha ya kupoteza fainali hiyo ninaweza kusema Zanzibar imekufa kiume kwanza kuanzia maandalizi, Zanzibar Heroes ilitumia usafiri wa basi kutoka Dar es salaam hadi Kenya kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo wakati Timu ya taifa ya Tanzania Bara ambao wanastahili kuitwa ‘vichwa vya Wendawazimu’ hao walitumia pesa nyingi za Watanzania kusafiri kwa ndege, ambapo hata hivyo licha kuondoka kwa mbwembwe wametolewa mapema kwenye michuano hiyo.

Zanzibar imetoa somo kubwa kwa Timu ya Kilimanjaro Stars ikiwemo uzalendo na Kujituma kwa ajili ya taifa, leo hii ukiangalia jinsi Wachezaji wa Kilimanjaro Stars walivyokuwa wanacheza uwanjani unaamini kabisa kuwa hawakuwa tayari kulitumikia taifa lao.

Ukiangalia kikosi cha Zanzibar Heroes kilichoshiriki kwenye michuano ya CECAFA huwezi kulinganisha uwezo wa mchezo mmoja mmoja na kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichojaa majina makubwa na yenye uzoefu wa michuano mikubwa.

Watanzania wamechoka kunung’unika kila siku huu ni muda wa Serikali kupitia wizara yake ya Michezo na TFF kukaa chini kutafakari kwa kina ni jinsi gani wataziokoa timu zetu za taifa kutoka kwenye aibu hii kwenye soka.

Hongereni Zanzibar Heroes kupoteza kwenu ni matokeo tu ya mpira wa miguu bila shaka ingekuwa jambo la kheri kurudi nyumbani kwa ndege na kupokelewa kwa shangwe kwani mlichotumwa mmekifanikisha kwa 50%.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents