Habari

Zanzibar kuimaliza Malaria

 

Zenji_Mp_Nohamedi_Salehe_Udawi_face

Katibu mkuuwa wizara ya Afya Zanzibar, Dr M. Saleh Udawi, akionyesha dawa ya Malaria ambayo ndiyo kwa mara ya kwanza ilizinduliwa kitaifa katika viwanja vya kufanyia mikutano Mtumbaku, Zanzibar katika mpango wa Upatikanaji wa dawa hizo katika maduka binafsi kwa bei isiyozidi sh 1000, na Hospitalini bule.

 

 

Katibu huyo alisema wananchi wa Zanzibar wasiogope kuzitumia dawa hizo kwakuwa si ngeni kwao, zilikuwepo hapo mwanzoni ila zimefanyika ukarabati upya ili kuziweka katika hari nzuri kwa utumiaji. Anasema miongoni mwa mabolesho hayo ni kupunguza wingi wa dozi, kutoka dozi ya siku tatu kwa vidonge 24, kwa sasa watakuwa wakitumia dozi ya siku tatu kwa vidonge sita, zikiwa na nguvu ile ile.

Pia amesisitiza kwamba dawa hizo zitauzwa chini ya shilingi 1000, kwa maduka ya madawa na Hospitali binafsi ili kila mmoja aweze kumudu, na duka lolote ama taasisi yoyote itakayouza dawa ‘hiyo kwa bei zaidi ya hapo taarifa ipelekwe kwenye vyombo husika.

Aidha alisema pia watu wengi wamekuwa wakidharau vitu vya bei nafuu kwa kudhani havina ubora, ila amesema kwa hilo ni tofauti kwani dawa hizo zimekuwa na ghalama kubwa kiasi cha kampuni ya ACTm, kujitolea kulipa baadhi ya gharama kubwa na ndogo kulipiwa na Serikali.

Alisema dawa hizo ambazo zipo katika mradi mmoja kama huo katika nchi nane, hazitatakiwa kutoka nje ya Zanzibar kutokana na makubaliano yao.

Zenji_dawa
Pia alisema dawa hizo katika kasha lake lina alama ya jani la kijani nembo na jina la ACTm, huku zikiwa katika hali tofauti kulingana na mtumiaji kuanzia uzito hadi umri. Dawa ya rangi ya poda inatumiwa na watoto wenye umri kuanzia miaka 2 hadi 11 wenye uzito wa 4.5 hadi 8 Kg.

Na dawa zenye rangi ya bluu wanatumia watoto wenye umri wa miaka 6 hadi 13 wakiwa na uzito wa 18 hadi 35 kg.

wakati rangi ya njano wanatumia watu wenye umri wa miaka 14 na kuendelea, na wenye uzito wa 35 kg na kuendelea
Zenji_Mh_Marick_Juma

Na Mkurugenzi wa kitengo hicho Marick Juma, alisema dawa peke yake si kitu ila lazima wafuate kanuni ya kuua mazalia ya mbu, kupiga dawa na kutumia chandurua ambavyo viligawiwa bule vyewe dawa ya mbu.
Zenji_wanafunzi
Wanafunzi wa Skuli za msingi wakifuatilia elimu hiyo ya Malaria.
Zenji_wazee
Wazee nao walikuwepo kwaajili kupata elimu hiyo.

Zenji_wanafunzi_wa_uuguzi

Wanafunzi wanaosomea fani ya uuguzi, wakiwa kama wadau wakuu katika kongamano hilo la kuimaliza Malaria Zanzibar
Zenji_watoa_dawa

Watoa huduma za dawa za Malaria wakisubili amri ya kuzinduliwa kwa dawa hiyo, na kupima watu papo hapo kwaajili ya kutoa dawa kwa mtu atakaye gundulika na malaria.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents