BurudaniHabari

Zanzibar Music Awards hiyoooo!!

Kituo cha Radio cha Zenji 96.8 FM cha mjini Zanzibar kwa mara ya kwanza ktk historia ya muziki wa kisiwa hicho,wanaandaa tuzo kwa ajili ya wanamuziki wa kisiwa hicho (Zanzibar Music Awards) zinazotarajiwa kufanyika tarehe 25 Feb 2006.

Taarifa kutoka kwa waandaji shughuli hilo zito zilisema dhumuni umuni kubwa la tamasha hilo kubwa ni kuonyesha kuthamini kazi za wanamuziki wa kizanzibari pamoja na utamaduni wa visiwa hivyo.

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa tamasha hilo linatarajiwa kuleta mwanga kwa utamaduni wa wazanzibari na kuongeza kuwa ni wanamuziki kutoka visiwani humo tu ndio watakaopata heshma ya kutunukiwa tuzo hizo.

Walizitaja categories zitakazotumika kuchagua washindi kuwa ni Taarab (Kidumbak, Asilia and Modern), Muziki wa Dansi,Drama pamoja na muziki wa kizazi kipya wa Zanzibar unaokuja kwa kasi sana (Zenji Flava).

Wasanii ambao wameshathibitisha kuperform siku hiyo wametajwa kuwa ni Mad Ice anayetamba na songi lake (Wange),Keisha na songi lake (Usinitenge & Zawadi) bila kumsahau mwanadada Renee Lamira. Hongereni wazanzibari kwa kuamua kujitoa mhanga na kujiandalia awards zenu…maana wabongo wamekuwa wakiwatosa sana kwenye Tanzania Music Awards sijui kwanini?????

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents