Michezo

Zanzibar yang’olewa uanachama wa CAF

Shirikisho la Soka barani Afrika limeinyang’anya Zanzibar uanachana wa Shirikisho hilo kwa kile lilichodai kuwa hakukuwa na utaratibu maalumu wakati wa uidhinishwaji wake.

Taarifa iliyotolewa na mtandao wa Shirikisho hilo zinasema Rais wa CAF, Ahmad Ahmad amesema kuwa  Zanzibar ambayo ni sehemu ya Tanzania haikupaswa kabisa kukubaliwa kuwa mjumbe wa 55, kwenye uamuzi uliofanywa Machi 2017 baada ya kupewa uanachama.

Aidha, Rais huyo amesema kuwa, Zanzibar ilikubaliwa kuwa mwanachama wa CAF bila kuzingatiwa kwa vigezo vya msingi ambavyo ni muhimu, huku akifafanua zaidi kuwa, CAF haiwezi kuvikubalia vyama viwili vya soka kutoka nchi moja yaani TFF na ZFA.

CAF imesema kuwa kigezo chao cha kutambua nchi ni ile inayotambuliwa na Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Umoja wa Mataifa (UN).

Licha ya kuwa Rais wa CAF aliyepita, Issa Hayatou aliikubalia Zanzibar kuwa mwananchama, lakini Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) lilikataa kuifanya Zanzibar kuwa mwanachama.

Zanzibar ni sehemu ya Tanzania lakini kwenye masuala ya mpira imekuwa ikijitegemea katika mashindano ya kanda, imekuwa ikishiriki kama nchi.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents