Habari

Zanzibar yataka kujiunga na OIC

BAADA ya awali Zanzibar kuzuiliwa kujiunga kwenye Jumuiya ya Kiislamu (OIC) baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi visiwani wameanzisha hoja hiyo na kutaka nchi yao iruhusiwe kujiunga na Jumuiya hiyo.

BAADA ya awali Zanzibar kuzuiliwa kujiunga kwenye Jumuiya ya Kiislamu (OIC) baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi visiwani wameanzisha hoja hiyo na kutaka nchi yao iruhusiwe kujiunga na Jumuiya hiyo.


Wajumbe hao waliokuwa wakitaka nchi yao kujiunga kwenye Jumuiya ya Kiislamu walidai kwamba sababu kubwa ni kutokana na mabadiliko yaliyopo ya sera ya mambo ya nje.


Wajumbe hao waliyasema hayo katika semina ya siku mbili ya kujadili sera mpya ya mambo ya nje, iliyofunguliwa juzi na Waziri wa Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha.


Mwakilishi wa Ziwani, Rashidi Seif alisema kwamba kutokana na kubadilika huko kwa sera kunaiwezesha Zanzibar kuruhusiwa kujiunga na OIC.


“mwanzoni Zanzibar ilizuiliwa kujiunga na Jumuiya hiyo kwa sababu za kisiasa lakini sasa kwa kuwa sera za mambo ya nje zimebadiliaka sasa ni wakati muafaka kuruhusiwa kujiunga,” alisema Seif.


Akijibu hoja hiyo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema suala hilo bado linazungumzika na linahitaji mjadala kati ya Visiwani na Bara.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents