Ze Comedy Wamalizana EATV

Lile kundi maaruku katika kituo cha luninga cha EATV la Ze Comedy ambalo limekuwa likiongoza katika kuchana mbavu za watu hapa nchini, hivi sasa halipo tena pamoja na kituo hicho baada ya kumaliza mkataba wao

Ze Comedy


 


Lile kundi maaruku katika kituo cha luninga cha EATV la Ze Comedy ambalo limekuwa likiongoza katika kuchana mbavu za watu hapa nchini, hivi sasa halipo tena pamoja na kituo hicho baada ya kumaliza mkataba wao na kugoma kuendelea kufanya kazi na kituo hicho huku wakidai wanataka kuangalia utaratibu mwingine wa kazi.



Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa kundi hilo bwana Issaya Mwakilasa a.k.a Wakuvanga alidai kuwa “hatuna matatizo kabisa na kituo cha EATV kwani tumefanya nao kazi katika kipindi chote hicho na wamekuwa wakitulipa vizuri sana hivyo hatuna budi kuwashukuru kwa hili, suala la kuacha kufanya kazi na EATV ni uamuzi wetu binafsi wala sio shinikizo la mtu yoyote tumeamua tu kuangalia taratibu nyingine” alisema.



Kundi hilo lilitokea kuwa maarufu sana linalowahusisha wasanii kama vile Joti, Mpoki, Mac Regan, Masanja, Vengu pamoja na Seki, limekuwa ni kitvutiokikubwa sana kwa jamii na kuna tetesi nyingi ambazo zinaendelea kuvuma mtaani zikidai kuwa inasemekana kuwa jamaa wana mpango wa kuangukia pande TBC jambo ambalo halina uhakika, kilichopo ni kutega sikio na kukodoa macho kwenye luninga itajulikana tu machizi wameangukia pande zipi?


 


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents