Bongo Movie

Zembwela apanga kuipanua Sanaa [Video]

Mwana maigizo na mchekeshaji mahiri Hilary Daudi ambaye anajulikana zaidi kwa jina la kisanii “Zembwela” leo ameongea na bongo5.com na kusema amejipanga vilivyo kurudisha heshima yake na ya Sanaa hiyo kwa kuandaa vitu moto moto ambavyo anaamini vitamuweka juu yeye pamoja na tasnia anayoifanyia kazi.

{hwdvs-player}id=1145|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

Akiongea na bongo5 nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam amesema kwa sasa amepumzika katika mchezo wa Mizengwe  na anajipanga kufanya sanaa kwa upana zaidi, mpaka sasa hivi tayari nimeshaandika  filamu  na komedi.

Zembwela ambaye ni mtunzi mashuhuri wa filamu za maigizo na vichekesho aliye na uwezo mkubwa kisanii alisema anaiomba serikali iwaruhusu  na kuwapa vibali  wasanii kutumia sehemu nyeti kama mahakama, polisi na mahospitali ili kuweka uhalisisia kwenye maudhui ya michezo na maigizo yao.

Vilevile aliyataka makampuni makubwa  kama mabenki na taasisi nyingine binafsi ziwapatie ruhusa ili kutumia ofisi zao  katika  kuigizia kwani itawasaidia wasanii  wa maigizo Sanaa ya uigizaji kukua na pia itapunguza gharamu kubwa katika kurekodi filamu zao.

“Kwa sasa nimeshaandaa filamu na komedi za kutosha nasubiria tu mambo yangu yakae sawa ili nitoe kazi zangu. Nina uhakika jamii itazipokea vizuri kwani nilizifanyia mazoezi na kujiandaa vya kutosha hivyo nawaomba wapenzi wa burudani na Sanaa za maigizo na vichekesho wakae mkao wa kula ”.

Zembwela ambaye alikuwa anajulikana zaidi kama mtunzi mkuu katika maigizo na tamthilia ya  Mizengwe katika kituo cha ITV alikuwa ndiye kiungo kikubwa katika kutunga, kuandika na kuongoza nini wenzake wafanye.

Akielezea kuhusu historia yake na maigizo Zembwela alisema yeye alianza kuigiza na  kutunga maigizo akiwa bado mdogo sana. “Nilianza shughuli hii wakati bado nipo shule ya msingi na nilikuwa najulikana kama baba cha kupewa”.

Nilikuwa nafanya mbwembwe Katika sherehe za mahafali ya kumaliza darasa la saba ambapo nilifanikiwa kutunga igizo moja zuri na la kusisimua lililoitwa “Radhi ya wazazi’, nikiwawakilisha vijana ambao wamesomeshwa kwa shida na wazazi alafu wakaja kuwadharau wazazi wao.

Zembwela  alichukua fursa hii kuwaasa wasanii wenzake wajiamini  kwani wao ni hela na sio na kupapatikia umaarufu, na wanapaswa kupata pesa na sio majina kwani umaarufu hau umpi mtu kula, nyumba wala maisha bora.

Akimalizia maongezi na Bongo5 Zembwela alisema matarajio yake yey ni kuwa mfanyabiashara maarufu katika tasnia ya Sanaa ya filamu nchini Tanzania.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents