Habari

Ziara ya Majaliwa yang’oka na watatu Singida, Yadaiwa waliajiriwa ‘kindugu’ ili waibe mapato

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Leo Jumatatu Oktoba, 7, 2019 amemwagiza Mkurugenzi Manispaa ya Singida, Bravo Lyapembile awaondoe kazini watumishi watatu wanaokusanya mapato kwenye stendi ya mabasi, Ambao inadaiwa wameajiriwa kindugu na wanatumiwa kuiba mapato.

Akitaja majina ya wakusanyaji mapato hao, Majaliwa amesema vijana hao waliowekwa kindugu ni Kennedy Francis (mtoto wa Mkurugenzi), Selemani Msuwa (ndugu yake diwani) na Salehe Rajab Kundya (shemeji yake diwani mwingine).

Andika barua leo hii hawa vijana waondoke kwenye hiyo kazi, na upeleke timu nyingine ya watu waaminifu, kuna mchezo unachezwa wa kukusanya mapato lakini hayapelekwi benki na wahusika wakuu ni mweka hazina wa Manispaa, Aminieli Kamunde na Mkaguzi wa Ndani, Ibrahim Makana,” Agizo la Majaliwa kwenda kwa Mkurugenzi Lyaembile.

Kwa upande mwingine, Majaliwa ametoa onyo kali kwa watendaji wa kata ambao wanakusanya mapato halafu hawapeleki fedha hizo benki na kupatiwa risiti.

Chanzo: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents