Habari

Ziara ya Rais Magufuli mkoani Lindi yaacha watu 51 mbaroni

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Lindi, inawashikilia viongozi 51 wa vyama 10 vya msingi (Amcos), vinavyodaiwa na wakulima wa ufuta wa mkoa humo Tsh. Milioni 486. 869 msimu wa mwaka huu.

Rais Magufuli

Akizungumza na waandishi wa habari jana Oktoba 18, 2019 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia. John Mbungo, amesema ukamatwaji wa viongozi hao ni utekelezwaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilotoa Jumanne ya Oktoba 15, mwaka huu katika mkutano wa hadhara wilayani Ruangwa.

Rais Magufuli aliimtaka Brigedia Mbungo na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, kuhakikisha vyama 10 vya msingi vinavyodaiwa na wakulima wa ufuta vinawalipa fedha hizo kabla ya msimu wa korosho kuanza.

Brigedia Mbungo aliwataja viongozi walioshikiliwa na Takukuru kuwa wa Chama cha Msingi cha Milindimo kinachodaiwa Tsh milioni 90.711, ambao ni Hemedi Kilete (Mwenyekiti), Saidi Mkwela (Katibu), Twahili Kileta (Karani), Hillard Chadill (Karani) na Hassan Lidemu (Karani).

Wengine wa Chama cha Msingi cha Mtonao kinachodaiwa Tsh. milioni 73.715 waliokamatwa ni Hasani Lingunja (Karani) na Karimu Ngara (Karani).

Pia Takukuru inawashikilia Zuber Nolele (Mwenyekiti) na Mjamari Kibohu (Katibu) kutoka Chama cha Msingi cha Kipelele kinachodaiwa Sh milioni 57.257.

Pia taasisi hiyo inawashikilia Hussein Mnindi ambaye ni Katibu wa Chama cha Kinjikitile ambacho kinadaiwa Sh milioni 15.1.

Wengine ni Saidi Mbunda (Makamu Mwenyekiti), Mathiad Likumwili (Mjumbe), Chande Madudu (Mjumbe), Issa Lutumno (Mjumbe) na Nasra Chingwile (Karani) wote kutoka Chama cha Msingi Nachiunga ambacho kinadaiwa Sh milioni 10.780.

Kwa upande wa Chama cha Msingi Chikonji kinachodaiwa Sh milioni 10.325, ni Abdallah Mtala (Mwenyekiti), Karimu Maguto (katibu), Hussein Hussen (mjumbe), Latifa Abdallah (karani) na Amina Mtauna (mjumbe).

Wengine wanaoshikiliwa ni Zainabu Khalifa (makamu mwenyekiti), Bashiri Ally (katibu), Abdallah Abdallah (katibu msaidizi), Haji Namanyanga (karani), Mohamed Ligoli (karani), Saidi Nguli (karani), Pius Lucas (karani) na Abrahamani Kapanda (karani) wote wa Chama cha Msingi Mtama kinachodaiwa Sh milioni 8.523 na fedha nyingine Sh 160,00.00 zinazodaiwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Lindi (Mwambao).

Pia wamo Ally Mtombo (katibu) na Mshamu Ngurangwa (karani) kutoka Chama cha Msingi Matumbi kinachodaiwa Sh milioni 12.154.

Wengine wanaoshikiliwa ni Nurdini Ndope (mwenyekiti), Shaibu Matumbi (katibu), Hamza Kumtitima (katibu msaidizi), Mustafa Chumbo (mjumbe), Selemani Mtonda (mjumbe) na Mponjila Mponjila (karani), wote kutoka Chama cha Msingi Ruangwa (Mandawa) kinachodaiwa Sh milioni 4.095.

Takukuru pia inawashikilia viongozi wa Chama cha Msingi Mchina kinachodaiwa Sh milioni 3.604 ambao ni Mussa Maringa (mwenyekiti), Jafari Likwena (makamu mwenyekiti), Patrick Martine (katibu), Abdallah Maringa (mjumbe wa bodi) na Hassan Mteremko (karani).

Katika Chama Cha Msingi Mnolela kinachodaiwa Sh milioni 3.052, wanaoshikiliwa ni Ismail Mkopi (mwenyekiti), Hamida Kaulu (makamu mwenyekiti), Masoud Hamisi (katibu), Nadhifu Nauka (katibu msaidizi) na Ismail Nauka (mjumbe).

Takukuru pia inawashikilia Said Mchia (mwenyekiti), Aziz Mchemba (katibu) na Abubakari Maharagwe (mjumbe), wote kutoka Chama cha Msingi Mmangawanga kinachodaiwa Sh milioni 3.314.

Kwa upande wa Chama cha Msingi cha Mageuzi kinachodaiwa Sh milioni 2.630, wanaoshikiliwa ni Saidi Mpili (mwenyekiti), Saidi Likotea (katibu) na Bakari Mpili (mjumbe).

Brigedia Mbungo alisema kati ya Sh milioni 436.869 zinazodaiwa na wakulima hao, watuhumiwa wamesharejesha Sh milioni 46. 416.

Alisema ufuatiliaji wa madeni ya wakulima utaendelea vyama vya msingi vya Nyangamara, Namangle, Nahuka, Mtua, Kigoli, Malungo, Madwanga, Nanjilinji, “A”, Zinga, Rutamba, Nyangamara, Naambu, Mbwemkuru na Mlindimo Mtunaho.

Brigedia Mbungo pia alitoa rai kwa viongozi wote wa vyama  vya ushirika nchini vinavyodaiwa na wakulima kulipa madeni yao kabla Takukuru haijawafikia kwani hakuna chama kinachodaiwa kitakachobaki salama.

CHANZO: GAZETI MTAMNZANIA

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents