Michezo

Ziara ya Zambia itawabeba Azam kwenye kombe la Shirikisho?

Timu ya Azam ni bingwa mtetezi kwenye mashindano maalum yaliyofanyika nchini Zambia, mashindano hayo yalizishirikisha timu nne, Zesco United, Zanaco FC, Azam FC na Chicken Inn.

8

Azam FC inaiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo wikiendi hii itacheza na timu ya Bidvest Wits kutoka nchini Afrika Kusini.

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, ambaye ameambatana na timu hiyo kuelekea huko Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo huo.

“Kwanza kabisa tunamshukuru Mwenyezi Mungu kuwa timu imewasili salama na jana (juzi) kulikuwa na mvua kubwa na timu iliweza kufanya mazoezi kwenye hali ya mvua, utakumbuka kuwa hali hii ndio tuliikuta tukiwa Ndola (Zambia) na wenzetu wa Zesco United walituambia hii ndio hali mtakayoikuta Afrika Kusini mwezi wa tatu, kwa hiyo tunashukuru sana kwamba ni hali ambayo sio ngeni kwetu kwa sasa hivi, ni hali ambayo tumefanyia mazoezi na kuchezea mechi,” alisema.

“Kwahiyo kwa maana ya mchezo kila kitu kinakwenda vizuri na tunaamini kabisa ya kwamba kesho (leo) ni siku ya mwisho ya mazoezi tutapata nafasi ya kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Bidvest kwa sababu ndio uwanja wa mechi na baada ya mazoezi kutakuwa na kikao cha benchi la ufundi na hivyo kufanya taratibu za mchezo kuwa zimekamilika kwa ajili ya kuchezwa,” aliongezea Kawemba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents