Aisee DSTV!
SwahiliFix

Zidane ajitapa baada ya kukutana na Pogba Dubai “Nilichoongea naye ni siri yangu” Ole Gunnar ajibu kuhusu hilo – Video

Zidane ajitapa baada ya kukutana na Pogba Dubai "Nilichoongea naye ni siri yangu" Ole Gunnar ajibu kuhusu hilo - Video

Ole Gunnar Solskjaer alisema”Sasa tunaendeshwa na picha! Sijamsikia Paul Pogba akisema hataki kuwa hapa. Paul anataka kukaa hapa na kucheza vizuri.” “Paul ni sehemu ya mpango wetu kwenda mbele na kuendelea nae,”

“Amekuwa akicheza hata kama akiwa na maumivu. Ametukanwa hata akicheza kushoto, kulia na hata katikati, lakini aliporudi dhidi ya Rochdale na Arsenal hakuweza kucheza kwa urahisi.

“Alitaka kucheza, alitaka kujaribu kurudi na alikuwa anaumia sana Alikuwa, yuko njiani kurudi na amekuwa mbali kwa siku chache, akifanya kazi lakini hayuko hapa.

“Halafu kuna picha na ukiwa ya Manchester United unapata picha na uvumi  lakini sina shida na hilo.”

Katika mkutano na waandishi wa habari Zindane al;izungumzia alipokutana na Pogba na kusema:- “Ni bahati nzuri,”

“Alikuwepo na nilikuwa pale kwenye hafla hiyo na, kwa kuwa tunajuaana, tulizungumza. Na yalikuwa ni mazungumzo ya kibinafsi,

“Sitaki kuwaambia tuliongea nini, hiyo ni kati yake na mimi. Lakini tumefahamiana kwa muda mrefu, kwa hivyo ikiwa tutakutana, tunasema lazima tusalimiane na tunazungumze angalau kidogo.”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW