Michezo

Zidane ambipu Mourinho London, atumia kibanda cha simu chenye rangi ya Man United na mkewe atupia uzi mwekundu 

Zinedine Zidane akiwa na mke wake Veronique wameonekana katika mitaa mbalimbali ya jiji la London huku wakipiga picha kwenye kibanda cha simu chenye rangi nyekundu ambayo ndiyo inayowakilisha klabu Manchester United ambayo amekuwa akihusishwa nayo katika siku za hivi karubuni kuwa huwenda akachukua mikoba ya Jose Mourinho.

Zidane ameposti picha hiyo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram inayomuonyesha akiwa na mkewe huku wakitumia simu kutoka kwenye kibanda cha rangi nyekundu ambayo wachambuzi wa soka wanaona kama ishara ya ‘kumbipu’ mpinzani wake Mourinho na kumtaka kujiandaa kung’atuka ili kurithi nafasi yake huku mashabiki wengi wa United wakisubiria kwa hamu tukio hilo baada ya kuchoshwa na matokeo mabovu wanayopata timu yao toka wakati wa maandalizi ya msimu huu.

Akiwa England katika ugawaji wa tuzo za FIFA, Zidane ambaye anamafanikio makubwa katika michuano ya Champions League kwa kutwaa mataji hayo mara tatu akiwa na Madrid amemshuhudia kocha wa timu yake ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps akitajwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo baada ya kukiongoza vema kikosi cha Ufaransa kwenye michuano ya kombe la Dunia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents