Michezo

Zidane na ndoto zake za Pogba ziko pale pale, Chelsea kuvunja rekodi yao ya usajili kwa nyota huyu

Manchester United wanaweza kumsajili kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate endapo watamtimua Ole Gunnar Solskjaer mwishoni mwa msimu. (Sun)  

kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate

Kocha msaidizi wa United Mike Phelan amesema klabu hiyo bado inataka kusajili wachezaji nyota. (Evening Standard)

Chelsea wapo tayari kuvunja rekodi yao ya uhamisho ili kumsajili mshambuliaji wa England na klabu ya Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19. (Goal)

Chelsea itapata majibu hii leo endapo marufuku waliopigwa ya kufanya usajili (kwa madirisha mawili) inayotarajiwa kuisha mwezi Februari kama itaondoshwa na kuruhusiwa kuingia sokoni mwezi Januari. (Daily Telegraph)

Image result for ZINEDINE ZIDANE is at loggerheads with his Real Madrid board as he pushes on with his bid to land £180million Manchester United midfielder Paul Pogba.

Kiungo wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane bado anataka kumsajili kiungo wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Marca)

Manchester City wanaamini kuwa mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 24, atasaini mkataba mpya na klabu hiyo utakaomfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi klabuni hapo. (Metro)

Liverpool na Arsenal wameungana na Barcelona katika kinyang’anyiro cha kutaka kumsajili mshambuliaji kinda wa Ujerumani Karim Adeyemi, 17 kutoka klabu ya RB Salzburg. (Sport via Mirror)

Everton wanajiandaa kumpa mkataba wa muda mrefu kwa beki wa kushoto wa Ufaransa Lucas Digne, 26. (Mail)Kocha wa Atletico Madrid ya Uhispania Diego Simeone

Kocha wa Atletico Madrid ya Uhispania Diego Simeone

Kocha wa Atletico Madrid ya Uhispania Diego Simeone, ambaye hapo kabla alikuwa akiwaniwa na klabu ya Everton ya England yu mbioni kuachana na miamba hiyo ya Uhispania. (Marca via Sport Witness)

Atletico wamekubali kumsajili kiungo machachari kutoka klabu ya Athletico Paranaense ya Brazili Bruno Guimaraes, 21, kwa dau la pauni 25.4m. (UOL, in Portuguese)

Tottenham wanapanga kumsajili beki wa kati wa klabu ya Norwich Ben Godfrey, 21, mwenye thamani ya pauni milioni 25. (Football Insider)

Tetesi bora za JumatanoAliyekuwa kocha wa Man United,Jose Mourinho na Kocha aliyetimuliwa na Tottenham Mauricio PochettinoAliyekuwa kocha wa Man United,Jose Mourinho na kocha aliyetimuliwa na Tottenham Mauricio Pochettino

Kocha aliyetimuliwa na Tottenham Mauricio Pochettino anataka kumrithi Ole Gunnar Solskjaer kama kocha wa Manchester United. (Manchester Evening News)

Tottenham wapo tayari kupokea ofa za usajili za chini ya pauni milioni 40 kwa kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 27. (Evening Standard)

Spurs haina mpango wa kumsajili kiungo Mserbia anayechezea Manchester United Nemanja Matic, 31. (Manchester Evening News)

Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) Aleksander Ceferin amesema teknolojia ya usaidizi ya mwamuzi ama VAR ni “uozo” japo “haiwezekani kurudi nyuma”. (Mirror)

Arsenal wamefanya mawasiliano na kocha wa zamani wa Valencia Marcelino wakati klabu hiyo ikiendelea kusaka kocha mpya wa kudumu. (Goal – in Spanish)

Kocha wa Tottenham Jose Mourinho ameacha kumfuatilia kiungo wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, 25, kutokana na kuwa na dau la pauni milioni 85 katika mkataba wake. (Mail)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents