Michezo

Zifahamu takwimu za Arsenal dhidi ya Liverpool kabla ya mchezo wao wa leo usiku ‘Arsenal hajapata ushindi ndani ya michezo 6 dhidi ya Liverpool’

Zifahamu takwimu za Arsenal dhidi ya Liverpool kabla ya mchezo wao wa leo usiku 'Arsenal hajapata ushindi ndani ya michezo 6 dhidi ya Liverpool'

Klabu mbili kongwe katika ligi kuu nchini Uingereza PL Liverpool dhidi ya Arsenal leo zinakutana kusaka alama muhimu tatu kila mmoja Liverpool wakiwa nafasi ya pili kwa alama 26 wakiwa sawa na vinara Man City ila tofauti ni magoli tu Man city wakiwa na magoli 26 huku Liverpool wakiwa na 16 wote wakiwa tayari wamecheza michezo 10 huku Arsenal wakiwa katika nafasi ya nne na alama zao 22.

Liverpool wakianzishwa mnamo mwaka 1892 miaka 126 hadi hivi sasa ikitokea katika jiji la Liverpool, wakitwaa taji la ligi hiyo kwa nyaka 18 tofauti huku ikiwa mara ya mwisho kutwa ilikuwa ni mwaka 1989-90 chini ya kocha Benitez, kwa jina la utani wakiitwa Majogoo wa Anfield, na uwanja wao ukiwa ni Anfield.

Arsenal wao walianzishwa mnamo mwaka 1886 mika 131 hadi hivi sasa ikitokea katika jiji la London, wakitwaa taji la ligi hiyo kwa nyakati 13 tofauti na mara ya mwisho kutwaa taji hili ilikuwa msimu 2003-04 chini ya kocha Arsene Wenger,jina la utani wakiitwa The Gunners uwanja wao ukijulikana kama Emirates, zamani ulikuwa Highbury.

Timu hizi mbili zimekutana mara 52 Arsenal wakishinda mara 15 nyumbani wakishinda mara 9 na ugenini wakishinda mara 6,huku Liverpool wakishinda mara 19 nyumbani wakishinda mara 12 na ugenini mara 7, na sare zikitoa mara 18, na katika mchezo wa leo usiku majira ya saa 2:30, timu hizi zinakutana kwa mara ya 53 katika dimba la Emirates ambalo ndio nyumbani kwa Arsenal.

Kati ya michezo ambayo inategemewaga kuwa na magoli mengi huu ni mmoja wapo kwani katika mchezo wa mwisho timu hizi zilitoa sare ya goli 3-3 katika uwanja wa Emirates,na katika takwimu zinaonyesha michezo 5 ya mwisho yalipataikana magoli 27,pia katika michezo hiyo mitano Liverpool ndio kashinda michezo mitatu huku Arsenal wakiwa hawakufanikiwa kushinda na michezo iliyobaki ikiwa ni sare.

Arsenal wanategemea kucheza mchezo wa 8 bila kufungwa huku Liverpool wakitegemea kushinda na kuwa miongoni mwa timu zinazoongoza ligi msimu huu wakimhofia sana Man city.

Taarifa za timu:

Arsenal: Matteo Guendouzi anaendelea kuwa nje huku Mohamed Elneny ataendelea kuwa nje kwa majeraha ya pua, Laurent Koscielny  majeraha ya Achilles na Dinos Mavropanos akiwa na tatizo la groin. Pia kuna mashaka juu ya Nacho Monreal akisumbuliwa na hamstring, Hector Bellerin tatizo la pua, Sokratis jeraha la mguu na Sead Kolasinac tatizo la hamstring.

Liverpool: Wachezaji na viungo wa Liverpool Jordan Henderson na Naby Keita wote wawili wana tatizo la hamstring hivyo watakosekana kwenye safari ya London, lakini pia kiungo wa zamani wa Gunner Alex Oxlade-Chamberlain akiendelea kusumbuliwa na goti.

Je..! Unajua ?

Arsenal wanausaka ushindi wa kwanza dhidi ya Liverpool ndani ya michezo 7 iliyopita ? (D3 L3), Roberto Firmino amefanikiwa kushinda na ku-assist katika michezo mitatu iliyopita dhidi ya Arsenal na kama atafanikiwa katika mchezo huu atakuwa mchezaji wa kwanza kufanya hivyo katika ya timu hizi mbili katika michezo minne mfululizo.

Jurgen Klopp hajapoteza katika michezo mitano dhidi ya Arsenal,Jose Mourinho pekee ndio mwenye michezo 12,Gerry Francis michezo 8, Alex Ferguson michezo 6.

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents