AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Zifahamu timu 24 zilizoungana na Tanzania kufuzu michuano ya Afcon 2019 Misri (+ Video)

Taifa Stars imefanikiwa kufuzu Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) kwa mara ya pili ikiwa ni maka 39 imepita tangu iingie kwenye michuano hiyo. Taifa Stars imefuzu kwa ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Uganda, ambapo Matokeo mengine Lesotho imetoa sare ya 0-0 dhidi ya Cape Verde.

Timu 24 zilizofanikiwa kufuzu Afcon 2019 Misri.

Goli la kwanza la stars lilifungwa na mshambuliaji Simon Msuva baada ya kupokea pasi kutoka kwa John Bocco. Mpaka mapumziko matokeo yalikuwa 1-0.

Magoli yote ya Taifa Stars dhidi ya Uganda

Dakika tano baada ya kipindi cha pili kuanza, Stars walipata penati baada ya mpira uliopigwa na nahodha Mbwana Samatta kutua kwenye mkono wa mlinzi wa Uganda Cranes Kirizistom Ntambi kwenye eneo la hatari.

Wachezaji wa Taifa Stars na makocha walivyoongea
Wachezaji walivyocheza Tetema, Askari apagawa na kocha amkumbatia

Mkwaju wa penati hiyo ulisukumwa nyavuni na mlinzi Erasto Nyoni na kuiandikia Stars bao la pili.Ushindi mnono kwa Stars ulihitimishwa katika dakika ya 57 mara baada ya beki Agrey Morris kufungwa kwa ustadi goli la kichwa akiunganisha krosi maridhawa iliyochongwa na John Bocco.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW