Habari

Zimbabwe: Wafanyakazi wa serikali kuandamana 

Wafanyakazi wa serekali nchini Zimbabwe wanapanga kuandamana Jumatano baada ya serekali kushindwa kuridhia madai yao ya kutaka walipwe mishahara inayokwenda sambamba na thamani ya dola ya Marekani.

Maandamano ya awali ya kupinga hali ngumu ya maisha mjini Harare, Zimbabwe

Polisi waliruhusu vyama vya wafanyakazi kufanya maandamano hayo ya kudai mishahara bora, jambo ambalo linatizamwa na wadadisi kama mtihani kwa rais Emmerson Mnangagwa, ambaye siku za hivi karibuni alipiga marufuku maandamano ya upinzani.

Kwa mujibu wa shirika la habar la Voice of America, Serikali imesema haina uwezo wa kulipa mishahara inayofuatana na thamani ya dola ya Marekani, hali ambayo itapelekea mfanyakazi anayepokea mshahara mdogo kulipwa dola ya Zimbabwe elfu 7,293, sawa na dola za Marekani 475 kwa mwezi, kuliko dola ya Zimbabwe 1,023 anazolipwa sasa.

Wafanyakazi wa Zimbabwe wanaathirika kutokana hali mbaya ya uchumi wa taifa, inayosababishwa kwa kiasi kikubwa na mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu, uhaba wa sarafu za kigeni, mafuta na dawa, pamoja na mgao wa umeme ambao unazorotesha shughuli za viwanda na uchimbaji madini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents