Burudani

Zimbabwe ya Roma haikamatiki YouTube, yavunja rekodi hii

By  | 

Video mpya ya wimbo, Zimbabwe ya Roma Mkatoliki iliyoachiwa August 10, 2017  inaendelea kufanya maajabu katika mitandao ya kijamii.

Video hiyo toka iachiwe ime-trend namba moja kupitia mtandao wa YouTube huku ikiwa na views 322,082 ndani ya masa 24.

Huwenda hii ndio video yake ya kwanza kufanya vizuri zaidi kwa muda mchache kupitia mitandao ya kijamii.

Huo ni wimbo wa kwanza toka rapa huyo atoke kwenye sakata la kutekwa.

Wadau wa mambo wanadai hali hiyo imesababishawa na rapa huyo kuliingiza suala la kutekwa ambalo lilileta mshikemshike nchini.

Rapa huyo pamoja na wenzake watatu walitekwa na watu wasiojulika na baada ya siku chache kuachiwa huku wakiwa na majeraha.

Mpaka sasa bado upelelezi kuhusu sakata hiyo bado unaendelea.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments